Ungana nasi kwa kuandika email yako hapa ili upate habari mpya kupitia email yako bila usumbufu:


Showing posts sorted by relevance for query MICHEZO. Sort by date Show all posts
Showing posts sorted by relevance for query MICHEZO. Sort by date Show all posts

TAMASHA LA MICHEZO LILILOANDALIWA NA WIZARA YA HABARI NA MICHEZO KWA KUSHIRIKIANA NA UBALOZI WA SERIKALI YA UINGEREZA NCHINI




 
 
 
 
 
TAREHE: 27, MACHI, 2012
MUDA: 4 Asb- 7 Mch
MAHALI: TCC CHANG’OMBE.


Wizara ya habari, Vijana Utamaduni na Michezo kupitia Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kwa ushirikiano na Ubalozi wa Uingereza nchini Kupitia shirika la British Council kwa miaka miwili wamekuwa wakiandaa na kuratibu Tamasha kubwa la Michezo linalofanyika mara moja kwa mwaka likiwa na malengo makuu mawili ambayo ni kuhamasisha ushiriki zaidi wa wasichana pamoja na wenye ulemavu katika michezo sambamba na kuwezesha asasi za serikali kushirikiana kwa karibu na wadau pamoja na asasi binafsi zinazojishughulisha na michezo pamoja na maendeleo ya vijana katika kutambulisha na kuonyesha baadhi ya shughuli wanazozifanya katika sekta hiyo nchini.

Kwa mwaka huu wa 2012, Wizara ya Habari Vijana Utamaduni na Michezo kupitia baraza lake linalojishughulisha na michezo nchini ‘Baraza la Michezo la Taifa-BMT’ kwa kushirikiana na shirika la British Council Tanzania pamoja na asasi shiriki za RIGHT TO PLAY, FEMINA HIP, pamoja na GNRC Africa, wamendaa Tamasha la Michezo litakalofanyika siku ya Jumanne ya Tarehe 27, Machi, 2012 katika viwanja vya Sigara (TCC) Chang’ombe kuanzia saa nne kamili asubuhi hadi saba na robo mchana.

Huku malengo makuu kwa mwaka huu yakiwa ni:
Kuainisha na kuenzi mahusiano mazuri baina ya serikali na sekta binafsi katika maendeleo ya michezo.
Kuhamasisha sera ya Michezo kwa wote.
Kutoa fursa kwa vijana,asasi mbalimbali katika kuonyesha na kubadilishana uzoefu kwenye tasnia ya michezo.
Kuadhimisha siku 122 kabla ya kufanyika kwa michezo ya London Olympic 2012.
Pamoja na Kutoa fursa kwa wadau mbalimbali kufanya harambee kupitia njia ya kuchangia vifaa vya michezo kwa shule zenye mahitaji maalum.

Katika hatua za Maandalizi ya Tamasha hili shule za sekondari na msingi zitakazoshiriki zimekuwa zikiendelea kufanya mashindano ya ndani ili kupata timu wawakilishi zitakazo chuana katika michezo ya fainali kwenye michezo ya VOLLEYBALL (Wavulana na Wasichana), MPIRA WA MIGUU (Wasichana),pamoja na RIADHA kuanzia tarehe 21,Machi.

Miongoni mwa shule (3)za sekondari zitakazoshiriki ni pamoja na Kibasila, Azania pamoja na Lord
Baden Powell.

Huku Shule za Msingi zikiwa Mbagala kuu, kizuiani, Kibonde maji kutoka wilaya ya Temeke na Ali Hassan Mwinyi, Mwl. Nyerere, Ndugumbi, Mikumi, pamoja na Mzimuni kutoka wilaya ya Kinondoni.

Mbali na kilele cha Michezo ya Fainali kwa michezo ya Volleyball, Mpira wa miguu kwa wasichana na Riadha (Shule za msingi na sekondari).

Pia kutakuwepo na:
michezo ya asili na kufurahisha kwa Watoto,Maonyesho ya namna ya kufundisha michezo ya riadha kwa Watoto.Pamoja na Mbio za wazi na kuhamasisha za maili moja kwa wote watakaoshiriki.

Katika Tamasha hili Mgeni rasmi anatarajia kuwa Waziri wa wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo - Mh. Dr. Emmanuel Nchimbi (M) Pamoja na wageni waalikwa:
UBALOZI WA UINGEREZA NCHINI ASASI MBALIMBALI ZINAZOJISHUGHULISHA NA MAENDELEO YA MICHEZO.

VYAMA VYA MICHEZO NCHINI:-
-Chama cha Michezo ya Olympic nchini- TOC
Chama cha Michezo ya Olympic kwa wenye ulemavu- Paralympic-TPC
-Chama cha Mpira wa miguu nchini-TFF
-Chama cha Mpira wa wavu nchini-TAVA
-Chama cha mchezo wa riadha nchini-TAA

Wadau, Wanamichezo, pamoja na wapenzi wote wa michezo mnakaribishwa.

Asante.

Mohammed A.Mvumbagu
KNY Timu ya Waandaaji
TUPE MAONI YAKO

Maalim Seif Akutana na Viongozi wa Vyama vya Michezo

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akizungumza na viongozi wa vyama vya michezo Zanzibar, kwenye mkutano na wadau hao ulifanyika Baraza la Wawakilishi la zamani. Kulia ni Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Zanzibar, Sharifa Khamis. 


Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akiwa na viongozi wa vyama vya michezo Zanzibar, kwenye mkutano na wadau hao ulifanyika Baraza la Wawakilishi la zamani 

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, ameiagiza Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Zanzibar kuwasiliana na Wizara inayohusiana na mambo ya Michezo Tanzania Bara ili kujadiliana juu ya namna ya kutatua changamoto za kimichezo ya kitaifa na kimataifa.

Maalim Seif ametoa agizo hilo baada ya kukutana na viongozi wa vyama vya michezo Zanzibar katika mkutano uliofanyika baraza la wawakilishi la zamani Mnazimmoja, ambapo wadau hao wa michezo walilalamikia ushirikishwaji mdogo wa wanamichezo wa Zanzibar katika michezo inayoiwakilisha Tanzania.

Amesema serikali ina nia thabiti ya kurejesha hadhi ya michezo Zanzibar ili kuirejeshea sifa yake ya kimichezo iliyokuwa nayo hapo awali.

Wadau hao wa michezo wamesema hadhi ya michezo imeshuka Zanzibar kutokana na sababu mbali mbali zikiwemo upungufu mkubwa wa viwanja vya michezo hasa ile michezo ya ndani (Indoor games).

Sambamba na hilo wadau hao wa michezo wamesema serikali iliidharau michezo na haikutoa mkazo unaostahiki kuwaendeleza wanamichezo na kuibua vipaji vya wanamichezo.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Zanzibar Abdillahi Jihadi Hassan amesema tayari Wizara yake imeshaanza mchakato wa kuwasiliana na Wizara ya Elimu Zanzibar wenye lengo la kurejesha michezo maskulini, ambayo itaibua vipaji ambavyo vitaendelezwa na kurejesha hadhi ya michezo Zanzibar.

Baadhi ya wadau hao wameiomba serikali kutodharau michezo ya asili ikiwemo mchezo wa karata, mchezo wa ng’ombe na kuogelea ambayo inaendana na utamaduni wa Zanzibar na husaidia pia shughuli za utalii.
TUPE MAONI YAKO

KAMPUNI YA BIA YA SERENGETI YATOA MILIONI 150 KUDHAMINI TUZO ZA MWANAMICHEZO BORA WA MWAKA (TASWA)



 Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano Kampuni ya bia ya Serengeti Teddy Mapunda akizungumza na waandishi wa habari kwenye klabu ya City Sports Lounge asubuhi hii wakati alipotangaza udhamini wa kampuni hiyo kwa tuzo ya mwanamichezo bora wa mwaka inayoandaliwa na chama cha waandishi wa habari za michezo TASWA Kulia ni Katibu Mkuu wa TASWA Amir Mhando na katikati ni Mwenyekiti wa TASWA Juma Pinto
Mwenyekiti wa TASWA Juma Pinto Kulia akitoa shukurani zake kwa kampuni ya bia ya Serengeti kwa kudhamni tuzo hizo mwaka huu, kutoka kulia ni Makamu mwenyekiti wa TASWA Maulid Kitenge, Nandi Mwiyombela Meneja miradi Endelevu SBL na Teddy Mapunda Mkurugenzi wa Mawasiliano SBL.

====  ======  =======  ======


Kampuni ya bia ya Serengeti imetangaza rasmi kudhamini kwa kitita cha shs 150M chama cha waandishi wa habari za michezo Tanzania (TASWA) katika tukio la kutoa tuzo kwa mwanamichezo bora wa mwaka.Hafla hiyo inatarajiwa kufanyika mapema mwezi ujao.

 Tukio hilo la kihistoria litafanyika katika ukumbi maarufu hapa jijini Dar es Salaam Diamond Jubilee tarehe 14/06/2012 ambapo zaidi ya wageni 500 wanatarajiwa kufurika kushuhudia tukio hilo.

Akihutubia mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es salaam leo, Mkurugenzi wa mahusiano na mawasiliano wa kampuni ya bia ya Serengeti bi. Teddy Mapunda, amesema maamuzi ya kudhamini tukio hilo kwa mara nyingine ni kuendelea kusaidia kuinua tasnia ya michezo hapa nchini. “Kufanya hivi ni sehemu mojawapo ya kuwatambua wanamichezo, lakini pia kupitia udhamini huu, tungependa kuwasaidia waandishi wa michezo kujaribu kuangalia ndani zaidi na kuleta mwanga na uelewa wa haraka kwa jamii juu ya michezo mbalimbali iliyopo hasa hapa kwetu Tanzania”alisema Mapunda.

 Udhamini huu utatumika katika maeneo mbalimbali kufanikisha sherehe hiyo kama vile chakula cha jioni, burudani,tuzo, vyeti, zawadi pamoja na mahitaji na matumizi mengine ili zoezi hili liwe nzuri na la kukumbukwa nchini”, aliongeza Bi. Mapunda.

Mkurugenzi huyo aliongeza kuwa kampuni ya bia ya Serengeti inajivunia kuwa mdhamini mkuu wa tuzohizi kwa mwaka wa tatu sasa. “sisi kamaSBL kwakweli tunajivunia kuwa wadau wa tukio hili kwa mara nyingine, lakini pia tunajivunia kuwa na waandishi bora wahabari za michezo ambao wamekuwa mstari wa mbele katika kuinua na kuendeleza tasnia ya michezo hapa nchini kupitia taarifa sahihi zenye kuelimisha jamii juu ya swala zima la michezo” .

 Naye Mwenyekiti wa chama hicho TASWA Bw.Juma Pinto, ametoa shukrani zake kwa niaba ya TASWA kwa kampuni ya bia ya Serengeti na kusema kuwa wana faraja kubwa kwa kuona kampuni kama SBL inajitolea na kuwasaidia mwaka hadi mwaka kwa miaka mitatu sasa. 

Alisema kwamba wanatambua umuhimu wa kampuni hiyo(SBL) katika kusaidia kuinua michezo hapa nchini, “sisi hatuwezi kusema kitu,zaidi ya kushukuru sana kwa SBL kwakweli ni dhahiri kabisa  kuwa SBL inaendelea kubadilisha taswira ya michezo hapa nchini kwa mengi na haswa kwa kudhamini tukio hili la kutoa tuzo kwa waandishi bora wa michezo.Wamebadilisha tukio hili kuwa la kimataifa”, alisema Pinto.P
TUPE MAONI YAKO

UDOM YAJIPANGA KUJENGA VIWANJA VYENYE UBORA ZAIDI

makamu mkuu wa chuo kikuu cha dodoma akisalimiana na wanamichezo mbalimabali wakati la bonanza lililofanyika juzi
 
KWA HABARI ZAIDI JUU YA BONANZA HILO ,BOFYA HAPA   <BONANZA>
 
CHUO Kikuu cha Dodoma (UDOM), kina mpango wa kujenga viwanja vya michezo vyenye ubora ili kuweza kukaribisha timu mbalimbali.

Hayo yalisemwa juzi na Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Idris Kikula wakati wa bonanza la michezo la Profesa Kikula lililofanyika katika chuo hicho mwishoni mwa wiki na kuoingeza kuwa mwaka huu chuo hicho kimefanikiwa kujenga viwanja vipya vya michezo na kilichobaki ni kuwekwa kwa chokaa.

“Michezo ni muhimu sana kwa wanafunzi, tutajitahidi kuwa na viwanja vingi ili wanafunzi wengi zaidi washiriki katika michezo mbalimbali, ikiwemo mpira wa miguu, pete, mpira wa wavu, na michezo mingine,” alisema

Alisema kuwa bonanza la mwaka huu limekuwa na mwamko mkubwa tofauti na mwaka uliopita kwani wengi wamejitokeza kushiriki mashindano hayo na kuwataka wanafunzi kuwa na tabia ya kushiriki katika michezo mbalimbali kwa lengo la kujenga uhusiano mwema na kuimarisha afya .

Mkufunzi wa michezo wa chuo hicho, Patrick Mwani alisema kuwa changamoto wanayokabiliana nayo ni upungufu wa vifaa vya michezo kutokana na chuo hicho kuwa na idadi kubwa ya wanafunzi ambao wanashiriki michezo.

Katika bonanza hilo, wafanyakazi na wanafunzi wa chuo hicho walishiriki michezo mbalimbali kama mpira wa miguu, netiboli, mbio za meta 100, mbio za magunia, kufukuza kuku na kuvuta kamba.
TUPE MAONI YAKO

HOTUBA YA NAIBU WAZIRI WA ELIMU ALIPOFUNGA CLINIC YA SPRITE HASHEEM THABEET 2012


 Mhe. Phillipo Mulugo (MB)Naibu Waziri wa Elimu akisoma hotuba yake
 Makamu wa Rais wa Shirikisho la Mpira wa kikapu Tanzania Phares Magesa
(Wa Pili Kulia,Brand Manager msaidizi wa Coca Cola Bibi Warda Kimaro(Wa Kwanza Kushoto)Afisa Utamaduni, Ubalozi wa Marekani,  Danna Banks(wa kwanza Kulia),Brand Manager msaidizi
 wa Coca Cola  Bibi Warda Kimaro(Wa Kwanza Kushoto),Hashim Thabeet(Wa Pili Kushoto)
 Baadhi ya Vijana Walioshiriki Clinic Ya Sprite Hasheem Thabeet 2012
---

Mkurugenzi wa Michezo,
Makamu wa Rais wa Shirikisho la Mpira wa kikapu Tanzania Ndugu Phares Magesa,Afisa Utamaduni Ubalozi wa Marekani, Danna Banks,Brand Manager msaidizi wa Coca Cola Bibi Warda Kimaro,Hasheem Thabeet ,Viongozi wa TBF,Makocha, 
Wachezaji na wadau wote wa michezo.

Kwa niaba ya Serikali na kwa niaba yangu binafsi napenda kuchukua nafasi hii  kuwashukuru TBF kwa kazi kubwa walioifanya ya kuakikisha mafunzo haya yanafanyika   katika kiwango kizuri , zaidi napenda kuwashukuru Coca cola kupitia kinywaji cha Sprite kwa kuendelea kufadhili mchezo wa Mpira wa kikapu hasa katika 
ngazi ya Vijana wadogo, pia nawashukru sana watu wa Marekani kupitia Ubalozi wao hapa Dar Es Salaam kwa kusaidia kuendeleza vijana wetu kupitia mchezo wa kikapu.

Kipekee na penda kumpongeza Hasheem Thabeet kwa kuonyesha thamani yake katika mchezo wa Mpira wa Kikapu na kukubali kutumia muda wake kwa ajili ya Vijana wadogo  kuwapa mafunzo na kuinua ari kwa vijana wetu  ili nao wapate kuwa na ndoto
 na  kufika pale alipo yeye

Nimatumaini yangu mafunzo haya mmeyapokea vizuri mtayazingatia na mtakapo rudi kwenye shule zenu nanyi mkawe mabalozi wazuri na walimu kwa wenzenu ambao hawakupata nafasi kama hii mliyoipataMikoa iliyoshiriki kliniki hii ya mwaka huu ni
Mwanza, Tanga, Dodoma,Kilimanjaro, Arusha, Unguja, Pemba na mkoa mwenyeji wa Dar es Saalaam hivyo basi ni matumaini yangu mwakani mikoa yote ya Tanzania bara na visiwani itashiriki, naomba wafadhili wajitokeze zaidi kuunga mkono jitihada za Cocacola na Hasheem Thabeet ili tuibue vipaji vingi zaidi katika kikapu.

Ndugu zangu serikali ipo pamoja nanyi katika michezo  kama mnavyofahamu wote kuwa mashindano ya Umiseta na umitashumta yamerudishwa rasmi mashuleni,   hivyo mafunzo haya waliyopata vijana hawa basi yatasaidia kuwaimarisha kimbinu za
kimchezo na ni matumaini yangu mikoa iliyoshiriki hapa itafanya vizuri kwenye mashindano yajayo ya shule za sekondari na msingi.

Serikali itaendelea kushirikiana na vyma vya michezo vyote nchini katika kuhakiksha michezo inaimarika mashuleni ikiwa ni pamoja kupeleka walimu wengi zaidi wakasomee  taaluma hii katika vyuo vyetu mbali mbali, ikiwa ni sambamba na kuongeza uwezo wa vyuo vyetu vya ualimu  kufundisha michezo.

Narudia tena wito wangu kuwa michezo ni sehemu muhimu ya kujenga vijana wetu kiafya, kielimu na kimaadili na hata kiuchumi hivyo basi ni jukumu la kila mmoja wetu, wanamichezo, wazazi, walezi na wakuu wa shule zote nchini kuhakisha vijana wanapatiwa fursa ya kushiriki katika michezo.

Nafahamu kuwa changamoto ya miundombinu ya michezo bado ni tatizo kubwa katika nchi yetu, hivyo basi Serikali itafanya kila jitihada kushirikiana na wadau wengine kuhakikisha tatizo hili linashugulikiwa ipasavyo katika ngazi zote.

Maombi yenu kwa serikali ya kuomba mpewe kipaumbele katika ujenzi wa uwanja mkubwa wa ndani wenye hadhi ya kimataifa kama wezenu wa soka na riadha wanavyofaidika na uwanja mkuu wa Taifa, nimeyachukua na nitayafikisha katika ngazi husika ili yaweze kushugulikiwa.

Nawashukuru sana wadhamini wa mafunzo haya kampuni ya Cocacola kupita SPRITE naHasheem Thabeet na nitoe wito kwa wanamichezo wengine Tanzania kuiga mfano wa Hasheem Thabeet wa kurudisha fadhila kwa jamii nzima ya watanzania na nia yake
 njema ya kuona vipaji vingine vinaibuka Tanzania.Niwatakie heri katika mafunzo mengine kama haya yatakyofanyika Arusha juma lijalo.

Natoa wito tena kwa makampuni mengine yajitokeze kudhamini michezo na hususani mchezo wa kikapu.
Niwatakie Safari njema wale wote watakaosafiri kurudi mikoani na niwashukuru wotekuanzia Walimu wenu,Wazazi kwa kuwapa ushirikiano mzuri katika kuchangia kufanikisha
malengo yenu.

Asanteni kwa kunisikiliza na sasa nimeyafunga rasmi mafunzo haya ya  SPRITE HASHEEM THABEET CLINIC 2012.

Mhe. Phillipo Mulugo (MB)
Naibu Waziri wa Elimu
TUPE MAONI YAKO

VODACOM TANZANIA YAIPIGA JEKI TAIFA QUEENS

Mke wa Waziri Mkuu Tunu Pinda pamoja na Kaimu Katibu Mkuu wa Chaneta Rose Mkissi wakipokea vifaa vya michezo kwa ajili ya timu ya taifa ya Netiboli-  Taifa Queens kutoka kwa Meneja wa Mahusiano ya Nje wa Vodacom Bw. Salum Mwalim.
 
 Vodacom imeipatia Taifa Queens vifaa mbalimbali vyenye thamani ya Shilingi Milioni Sita kuwezesha ushiriki mzuri wa timu hiyo kwenye mashindano ya Afrika yanayoanza kesho (Jumanne Mei 8, 2012) jijini Dar es salaam. Wa kwanza kulia ni mjumbe wa kamati ya maandalizi ya mashindano Shiza Mwakatundu
 
Mke wa Waziri Mkuu Tunu Pinda akipokea sehemu ya vifaa vya michezo vyenye thamani ya Shilingi Milioni Sita kutoka kwa Meneja wa Mahusiano ya Nje wa Vodacom Bw. Salum Mwalim kwa ajili ya kuiwezesha timu ya Taifa ya Netiboli Taifa Queens kushiriki vema mashindano ya Afrika kwa mchezo huo yanayoanza kesho jijini Dar es salaam. Vifaa hivyo vimejumusiha Suti za Michezo, viatu na Jezi. Kutoka kulia ni Mjumbe wa kamati ya maandalizi Shiza Mwakatundu na Kaimu Katibu Mkuu wa CHANETA Bi. Rose Mkisi
--
Kamapuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania leo imeipiga jeki timu ya taifa ya Netiboli - Taifa Queens kwa kuipatia vifaa mbalimbali vya michezo vyenye thamani ya shilingi milioni sita kuiwezesha timu hiyo kushiriki vema mashindano ya Afrika yanayoanza kesho jijini Dar es salaam.

Vifaa hivyo ni suti za michezo jozi 20, viatu vya michezo jozi 20, jezi seti mbili, BiBs 20 vyote vikiwa na thamani ya Sh. Milioni Sita na kukabidhiwa leo kwa Mke wa Waziri Mkuu Tunu Pinda kutoka kwa Meneja wa Mahusiano ya Nje wa Vodacom Tanzania Bw Salum Mwalim katika hafla fupi iliyofanyika kwenye makazi ya Waziri Mkuu jijini Dar es salaam
 
Akipokea vifaa hivyo Mama Pinda ameishukuru Vodacom kwa kuunga mkono juhudi za kuyawezesha mashindano hayo kufanyika vema chini ya uenyeji wa Tanzania kupitia chama cha Netiboli nchini – CHANETA.
 
“Nawashukuru sana Vodacom mmetupatia zaidi ya kile tulichowaomba, hii sasa ni wazi timu yetu ya Taifa Queens itafanya vizuri na kuibuka mshindi wa mashindano hayo makubwa kwa netiboli Afrika”Alisema Mama Pinda.
 
Kwa upande wake Bw. Mwalim alimpongeza Mama Pinda kwa kuwa mstari wa mbele kuhakikisha mashindano hayo yanafana chini ya ardhi ya Tanzania
 
“Kwa kweli mama umefanya kazi kubwa na nzuri sana inayostahili kila aina ya pongezi ya kuzunguka kila mahali kuhamasisha watanzania kuyachangia mashindano haya na timu yetu ya taifa – Taifa Queens, hakika umeonesha mfano mzuri na wa kuigwa kwamba Netiboli ikisimamiwa kidete kama ulivyofanya nayo chati yake itakuwa juu”Alipongeza Bw. Mwalim.

Bw. Mwalim aliongeza kusmea kuwa Vodacom siku zote inajivunia ushiriki wake katika kukuza michezo nchini ikitambua kuwa michezo ni eneo muhimu la kuwaunganisha watanzania na kuwapatia  wakati wa furaha baada ya pirika za hapa na pale
“Vodacom tunajivunia rekodi yetu ya kuendeleza na kukuza michezo nchini leo taifa zima linapongezana na kupena pole kufuatia mechi ya jana ya Simba na Yanga hayo ni matunda ya Vodacom kuweka udhamini katika soka na leo tunajivunia kuiwezesha Taifa Queens kushiriki mashindano ya kimataifa”Alisema Bw. mwalim
Mwisho
TUPE MAONI YAKO

Ziara ya Mh. Makala jimboni kwake

Mbunge wa Jimbo la Mvomero, Amos Makalla, ambaye ni Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, akioneshwa eneo la ujenzi wa soko la kisasa katika Kijiji cha Mvomero, Kata ya Mvomero , kabla ya kuwahutubia wananchi wa Kata hiyo , Mei 16, mwaka huu.
Mbunge wa Jimbo la Mvomero, Amos Makalla, ( mwenye Kaunda suti) ambaye ni Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, akiangalia hatua za ujenzi wa shule ya sekondari ya watoto wa wafugaji katika Kijiji cha Wafugaji cha Mela, Kata ya Melela, Wilayani humo Mei 18, mwaka huu alipofanya ziara ya kuangalia shughuli za maendeleo ambapo aliahidi kuwaunga mkono kwa kuwapatia misaada mbalimbali kwa ajili ya ujenzi.
Baadhi ya akina mama wa jamii ya wafugaji wa Kimasai wa Kijiji cha Mela, Kata ya Melela, Wilaya ya Mvomero, Mkoa wa Morogoro, wakimwimbia nyimbo za kumkaribisha Mbunge wa Jimbo hilo, Amos Makalla ( hayupo pichani) ambaye ni Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo alipofanya ziara yake Mei 18, mwaka huu Kijijini hapo.
Makamu Mkuu wa Shule ya Sekondari Nassor Seif ,Rehema Kapinga ( kushoto) akipokea seti moja ya Kompyuta yenye thamani za zaidi ya sh: milioni moja ukiwa ni msaada kutoka kwa Mbunge wa Jimbo la Mvomero, Amos Makalla, ambaye ni Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, wakati wa mkutano mkuu uliofanyika Mei 16, mwaka huu , eneo la Madizini katika Kata ya Mtibwa.
Mbunge wa Jimbo la Mvomero, Amos Makalla, ambaye ni Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, akipewa zawadi ya kuku ‘jogoo’ kutoka kwa Mama wa Kimasai , Sarah Bakari alipofanya ziara kwenye Kijiji cha Wafugaji cha Mela, Kata ya Melela, Wilayani humo Mei 18, mwaka huu na kuaahidi kuwapatia misaada mbalimbali kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya Sekondari ya watoto wa wafugaji .
Mbunge wa Jimbo la Mvomero, Amos Makalla, ambaye ni Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, akionesha kopi ya hundi y ash: milioni tano kwa wananchi wa Kata ya Kibati ,baada ya kuidhinisha kutoka mfuko wa Jimbo ili kuanza ujenzi wa soko la kisasa wakati alipokuwa akiwahutubia Mei 17, mwaka huu ikiwa ni mpango mkakati wa kuwainua wakulima wawezekuuza mazao kwa faida.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya Sekondari Mtibwa, wakiimba nyimbo za kumsifu MBunge wa Jimbo la Mvomero Amos Makalla, ambaye ni Naibu Waziri wa Habari, Vijana , Utamaduni na Michezo baada ya kuwasili shuleni hapo Mei 17, mwaka huu kuwasalimu , Mbunge huyo ameisaidia vifaa mbalimbali Shule hiyo ikiwemo na safaruji na mabati wakati wa ujenzi wa vyumba vya madarasa .
Mwenyekiti wa Kwaya ya Vijana wa Mtibwa wa Kanisa la KKKT, Rick Lucas ( kulia) akimkabidhi zawadi ya mbuzi Mbunge wa Jimbo la Mvomero, Amos Makalla, ambaye ni Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, ikiwa ni ishara ya kuonesha upendo kwake na kumpongeza kwa kuteuliwa na Rais Jakaya Kikwete kushika wadhifa wa Naibu Waziri wakati wa hafla fupi iliyofanyika Mei 17, mwaka huu eneo la Madizini.
TUPE MAONI YAKO

TASWA YAOMBOLEZA KIFO CHA MHARIRI WA MICHEZO WA GAZETI LA MTANZANIA, RACHEL MWILIGWA

Mhariri wa Habari za Michezo wa gazeti la Mtanzania, Marehemu Rachel Mwiligwa enzi za uhai wake.

CHAMA cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) kinaungana na familia na wanahabari wote nchini kuomboleza kifo cha Mhariri wa Habari za Michezo wa gazeti la Mtanzania Rachel Mwiligwa

TASWA imeshtushwa taarifa za kifo cha Rachel kilichotokea usiku wa kuamkia leo, hivyo tunatoa pole kwa familia yake, waandishi wa habari za michezo na wafanyakazi wenzake wote, wasanii na wanamichezo wengine katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mdau mkubwa wa michezo na burudani.

Kutokana na msiba huo, chama kinaandaa taratibu zake za kuwasilisha rambirambi kwa namna tulivyojiwekea, kwani marehemu hadi mauti yanamkuta alikuwa mwanachama mtiifu wa TASWA. Hivyo upo utaratibu kama mwenzetu akitangulia mbele ya haki namna gani tunatakiwa tufanye.

Lakini pia upo utaratibu mwingine nje ya chama ambao utahusu mtu binafsi kuwasilisha michango ya rambirambi, ambapo TASWA inawasiliana na wahariri wote wa habari za michezo wasaidie kukusanya michango ya rambirambi kwenye vyombo vyao, ambayo wataiwasilisha kwa wajumbe wa Kamati Maalum ya kusimamia jambo hili.

Wajumbe hao ni Angela Msangi ambaye atakuwa Mratibu akisaidiwa na Mwani Nyangasa, ambao watashirikiana na wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya TASWA, George John ambaye ni Katibu Msaidizi wa TASWA, Grace Hoka na Alfred Lucas ambao ni Wajumbe wa Kamati ya Utendaji. Tunaomba ushirikiano wa wadau katika kufanikisha jambo hili.

Msiba kwa sasa kwa mujibu wa taarifa za awali upo Manzese Tiptop,tutaendelea kujulishana kadri zitakavyopatikana taarifa mpya.

Tunaomba waandishi wa habari za michezo, wasanii na wanamichezo kwa ujumla tumuenzi Rachel kwa masuala mbalimbali aliyokuwa akiyatilia mkazo ikiwemo kusimamia ukweli kwa kile alichokiamini na ndio maana tunasema tutaendelea kumkumbuka daima. Mungu amuweke mahali pema peponi. Amin
Imetolewa na:
Amir Mhando
Katibu Mkuu TASWA
11/05/2012
TUPE MAONI YAKO

Bondia wa Tanzania Selamani Kidunda apoteza mchezo wake wa kwanza katika mashindano ya Olimpiki

Wadau wa michezo walioko London, kutoka kushoto Ndg. Amosi Msanjila afisa wa ubalozi London, Mtangazaji maarufu wa BBC Ndg. Charles Hilary, Makamu wa Rais wa TBF Ndg. Phares Magesa, na Mchambuzi mahiri wa Michezo wa BBC na mmliki wa tanzaniasports.com Ndg. Israel Saria.
Baadhi ya viongozi wa michezo walioko London, kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa michezo nchini Ndg.Thadeo, Rais wa Kamati ya Olimpiki Tanzania Ndg.Gullam, Makamu wa Rais wa Kikapu Tanzania Ndg.Magesa na Kiongozi wa msafara wa timu ya Tanzania Ndg. Jarufu.
Bondia wa Tanzania Selamani Kidunda mwenye fulana nyekundu akiwa na viongozi na baadhi ya wadau wa michezo wakati akienda kupigana na Bondia toka Moldova BELOUS Vasilii, Kidunda alipoteza mchezo huo kwa point 7-20.
Bondia Kidunda, mdau wa michezo Magesa na kiongozi wa msafara wa Tanzania Jarufu wakiwa kwenye basi la wanamichezo kurudi kambini.

Bondia pekee anayeiwakilisha Tanzania kwenye michezo ya Olimpiki Selemani Kidunda amepoteza mchezo wake leo dhidi ya Bondia BELOUS Vasilii toka Moldova kwa point 7-20.

Tanzania itajaribu tena bahati yake tarehe 31/07/2012 wakati muogeleaji wetu wa kiume Ammaar Ghadiyali atakapocheza mchezo wake, tumuombee kila la heri kijana huyo atuwakilishe vyema.
TUPE MAONI YAKO

Waziri wa Habari, Vijana,Utamaduni na Michezo Dk Fenella Mkangalla Kikosi Cha Timu ya Twiga Stars Kinayotarajiwa Kucheza Mchezo wa Marudiano na Timu ya Ethiopiia.

 Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mkangalla akisalimiana na mmoja wa Kamanda wa kikosi cha Jeshi la kujenga Taifa cha Ruvu JKT wakati alipokwenda kutembelea kikosi cha Timu ya Tiwiga Stars kinayotarajiwa kucheza mchezo wa marudiano na timu ya Ethiopiia.
 Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mkangalla akisalimiana na Kaimu Kamanda wa Kambi ya Kikosi cha Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) cha Ruvu Meja Alex Kakwaya wakati alipokwenda kutembelea kikosi cha Timu ya Tiwiga Stars kinayotarajiwa kucheza mchezo wa marudiano na timu ya Ethiopiia.
 Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenela Mkangalla akisisitiza jambo kwa kikosi cha Timu ya Taifa ya Twiga Stars (hawapo Pichani) wakati alipotembelea kikosi hicho kilichopo mazoezini kujiandaa na mchezo wa marudiano na timu ya Ethiopia kwenye kambi ya Jeshi la Kujenga Taifa Ruvu JKT, Kulia kwake ni Kaimu Kamanda wa Kambi ya Kikosi cha Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) cha Ruvu Meja Alex Kakwaya na kushoto kwake ni Luteni Rhoda Matonya.
 Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenela Mkangalla akiteta  jambo na  Kaimu Kamanda wa Kambi ya Kikosi cha Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) cha Ruvu Meja Alex Kakwaya wakati alipokwenda kutembelea kikosi cha Timu ya Twiga Stars kinachotarajiwa kucheza mchezo wa marudiano na timu ya Ethiopiia.
 Kaimu Kamanda wa Kikosi cha Jeshi la Kujenga Taifa cha Ruvu (JKT ) Meja Alex Kakwaya akiteta jambo na Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Michezo Bi. Juliana Yassoda wakati ugeni wa Wizara ulipokwenda kutembelea kikosi cha Timu ya Twiga Stars kilichopo mazoezini kujiandaa na mchezo wa marudiano na timu ya Ethiopia kwenye kambi ya Kikosi cha Ruvu JKT.
Baadhi ya Wachezaji wa Kikosi cha Timu ya Taifa ya Twiga Stars wakimsikiliza Mheshiiwa Dkt Fenella Mkangala wakati alipowatembelewa kwenye kambi ya Kikosi  cha Kambi ya Jeshi la Kujenga Taifa Ruvu JKT jana.Picha na Benjamin Sawe-Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
TUPE MAONI YAKO

MURJI ACHANGIA SAFARI YA WANAMICHEZO WA CHUO CHA UTUMISHI WA UMMA-MTWARA

Mbunge Jimbo la Mtwara Mjini,Mh.Hasnein Murji (kulia) akikabidhi pesa taslim kiasi cha sh. Mil. 1 kwa Kaimu Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma mkoani Mtwara,Bw Seme Peter wakati wa hafla fupi ya kukabidhi vifaa vya michezo Chuoni hapo.
Mh. Mbunge akikabidhi jezi kwa ajili ya timu ya Chuo hicho.
Baadhi ya wanafunzi wa Chuo hicho.

WACHEZAJI wa timu ya Chuo cha Utumishi wa Umma mkoani Mtwara wameombwa kudumisha nidhamu ya Michezo watakapokuwa katika mashindano ya michezo ya Vyuo vya Utumishi wa Umma nchini yatakayotarajia kufanyika mwanzoni mwa wiki ijayo Mkoani Tanga Wito huo umetolewa katika hafla fupi ya kukabidhiwa vifaa vya michezo na Fedha taslimu tsh Milioni moja toka kwa Mbunge wa Jimbo la Mtwara
mjini,Bw Hasnein Murji kwa lengo la kusaidia timu hiyo ili iweze kufanya vizuri na kutwaa ushindi katika mashindano hayo.

Akikabidhi vifaa hivyo Murji pia amehaidi kutoa Tshs Milioni Moja kwa kila mchezo utakaopata ushindi na kutwaa kikombe huku akidai kuwa atatoa Mabasi yake 10 kubeba wananchi kwa ajili ya Mapokezi kuanzia Mkoani Lindi watakapokuwa wanarudi na Vikombe.

Aidha mkuu wa chuo cha utumishi tawi la Mtwara ,Bw Seme Peter alisema kuwa kitendo kilichofanywa na mbunge huyo ni cha kuigwa kwani msaada huyo utaweza kuwasaidia wanamichezo na kuwapo moyo.

Kufuatia msaada huo,Rais wa Serikali ya wanachuo wa Utumishi Mtwara,DAISY JAFARI pamoja na NAHODHA wa Timu ya mikono ambae pia ni Naibu waziri wa Michezo Chuoni,Bi Moza Nassor kwa pamoja wakiongea na mdau wa blog hii waliwakikishia wana chuo pamoja na Wana Mtwara kuwa timu zao zitarudi na Ushindi kutokana na Ushiriano waupatao katika maandalizi

Michezo hiyo itakayoanza April 03 na kumalizika April 06 mwaka huu,Jijini Tanga na kushirikisha wanamichezo 50 kutoka kla Tawi la Chuo cha Utumishi wa UMMA kwa Michezo ya Mpira wa Miguu,Mpira wa pete,Volley ball na mpira wa kikapu
TUPE MAONI YAKO

HII NDO KAULI YA SUGU ILIYOSABABISHA BUNGE LISITISHWE GHAFLA LEO KUOGOPA UCHOCHEZI

Muda mfupi uliopita spika wa bunge, Anna Makinda amelazimika kusitisha shughuli za bunge mwanzoni tu mwa hotuba ya kambi rasmi ya upinzani iliyokuwa ikisomwa na waziri kivuli wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Joseph Mbilinyi aka Sugu.

Kauli kwenye hotuba hiyo iliyobabisha spika wa bunge asitishe shughuli za leo hadi jioni ilisema, 

“Tanzania imegeuka chini ya usimamizi wa wizara ya serikali hii ya CCM kuwa taifa linaloteka nyara wanahabari, kuwatesa, kuwangoa kucha na meno, kuwatoboa macho, kuwamwagia tindikali na hata kuwaua.”

SEHEMU YA HOTUBA  HIYO:

MKUU WA KAMBI YA UPINZANI MHESHIMIWA JOSEPH O. MBILINYI (MB) KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO KWA MWAKA WA FEDHA 2013/2014

(Inatolewa chini ya Kanuni ya 99(9) ya kanuni za Bunge toleo la mwaka 2013)
1. UTANGULIZI

Mheshimiwa Spika,


Dira ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo ni “kuwa na taifa lililohabarishwa vizuri, lina vijana wenye uwezo na malezi bora, linathamini utamaduni wake na linakuwa mahiri katika michezo ifikapo mwaka 2025.” Aidha, ‘dhamira’ ya wizara hii ni ‘kuendeleza utambulisho wa taifa kwa kuwezesha upatikanaji mzuri wa habari, kuwawezesha vijana kiuchumi na kukuza utamaduni na michezo kwa umma kwa maendeleo ya kijamii na kiuchumi.’


Mheshimiwa Spika,


Kwa maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Serikali hii ya CCM imeshindwa kutekeleza dira na dhamira iliyotajwa katika maandiko ya kisera ya Wizara. Badala yake, chini ya usimamizi wa Wizara hii, Tanzania imegeuka kuwa taifa lisilotaka watu kuhabarishwa vizuri juu ya matendo ya watawala. 


Tanzania imegeuka kuwa taifa linalofungia magazeti yanayofichua ufisadi, uchafu na matumizi mabaya ya madaraka miongoni mwa viongozi, watendaji na watumishi wa Serikali hii ya CCM. Tanzania imegeuka, chini ya usimamizi wa Wizara na Serikali hii ya CCM, kuwa taifa linaloteka nyara wanahabari, kuwatesa kwa kuwang’oa kucha na meno, kuwatoboa macho, kuwamwagia tindikali na hata kuwaua. 

Tanzania sio nchi inayoandaa vijana wake tena. Haiwapi tena elimu bora wala kuwapatia maarifa, uwezo na malezi bora; ni nchi isiyowawezesha wala kuwathamini vijana wake; ni nchi inayoruhusu vijana wake kunyonywa na kutoendelezwa; na ni taifa ambalo limeachia utamaduni utambulisho wake kama taifa kupotea kabisa. Aidha, katika fani ya michezo ya aina zote, Tanzania imeporomoka kutoka taifa lililokuwa linaheshimika kimataifa katika miaka ya sabini na kuwa alichokiita rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi, ‘kichwa cha mwendawazimu’ ambacho kila kinyozi anajifunzia kunyolea!


2. UHURU WA UHARIRI NA USALAMA WA WANAHABARI


Mheshimiwa Spika,


Kwa masikitiko makubwa, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inalitaarifu Bunge lako tukufu kwamba sasa Tanzania imeingia rasmi katika orodha ya fedheha (The List of Shame) ya mataifa ambayo taaluma ya habari ni taaluma ya hatari kwa wale wote wanaoitumia kama sehemu ya wajibu wao kwa taifa na kama ajira yao. 

Kwa mujibu wa taarifa ya Kamati ya Kulinda Waandishi wa Habari Ulimwenguni (the Committee to Protect Journalists - CPJ) iliyotolewa mwaka huu 2013, kwa mara ya kwanza tangu kuanzishwa kwa CPJ mwaka 1992, Tanzania imeingizwa kwenye orodha ya nchi 20 ambazo ni hatari kwa waandishi wa habari kufanya kazi zao kutokana na hatari ya kuuwawa kwa mwaka 2012 (20 Deadliest Countries in 2012). Kwa mujibu wa taarifa hiyo, ilishikilia nafasi ya 7 ulimwenguni kati ya nchi 20 zinazoongoza kwa kuhatarisha maisha ya waandishi wa habari.

Mheshimiwa Spika,


Kwa mujibu wa taarifa ya CPJ, tishio kubwa kwa waandishi wa habari duniani ni kuuwawa kwa kutekwa na kuteswa na/au kutishiwa maisha. Aidha, Serikali na vyombo vyake vya ulinzi na usalama ni washiriki wakubwa wa mauaji ya waandishi wa habari. 

Kwa mujibu wa takwimu za CPJ, kati ya waandishi waliouwawa mwaka 2012, karibu ya 20% waliuwawa ama na maafisa wa serikali au na majeshi yake. Karibu idadi hiyo hiyo ya waandishi wa habari waliuawa kwa sababu ya kufuatilia taarifa za kiuchunguzi na za hatari. Taarifa hiyo inaonyesha kwamba hadi kufikia Aprili 2013, waandishi wa habari wapatao 30 tayari wamekwishauawa ulimwenguni wakati wakitimiza wajibu wao; wakati mwaka 2012 waandishi wa habari 103 waliuwawa ulimwenguni kote.

Mheshimiwa Spika,

Taarifa ya CPJ inaungwa mkono na ushahidi wa matukio mengi yanayodhihirisha kwamba maisha ya waandishi wa habari wa Tanzania yako hatarini kutokana na vitendo na vitisho kutoka kwa Serikali na watendaji wake ambao hawataki kusikia ukweli dhidi yao ukianikwa hadharani. Kudhihirisha kauli hii tunaomba kumnukuu mwanahabari mahiri na mmoja wa wahanga wa vita dhidi ya wanahabari na uhuru wa habari hapa nchini, Mzee Ndimara Tegambwage:

“Mwaka 2006, waliojiita wananchi wakazi wa jiji la Mwanza, walikusanywa na wenye uwezo kufanya maandamano makubwa kwa walichoita ‘kupinga mwandishi Richard Mgamba kuandika uongo’ na kudai kwamba alikuwa Mkenya na ‘siyo raia wa Tanzania.’ Desemba 2009, mwandishi Frederick Katulanda wa Mwanza, alivamiwa nyumbani. Wavamizi walikuwa wakipaza sauti na kudai kuwa ana nyaraka za akaunti za benki za Halmashauri ya Jiji la Mwanza. Walikuwa na mapanga. Walikuwa wakichagizana kwa kusema, “Kata kichwa! Kata kichwa!” Waliondoka na mafaili. Walimwachia kilema mguuni na makovu mikononi.


“Mwezi Septemba, 2010 wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu, katika eneo la Nyambiti, Jimbo la Sumve wilayani Kwimba, mkoani Mwanza, mwandishi Frederick Katulanda alivamiwa na kupigwa na watu wapatao 15 waliojiita “Green Guard” - wa “chama cha kijani.” Katika “kumshughulikia,” Katulanda anasema, walikuwa wakionyesha kuwa na ujuzi mkubwa wa judo na karate huku wakidai kuwa anawaandika ‘vibaya’ Chama Cha Mapinduzi (CCM).


“Mwaka 2011 mwandishi Richard Massatu alikutwa amekufa katika eneo la Igoma, jijini Mwanza. Vyombo vya habari viliripoti kuwa macho yake yalikuwa yametobolewa na kuwekwa gundi aina ya super glue; mguu wa kushoto na mbavu vilikuwa vimevunjika. Vyombo vya habari viliripoti kuwa Massatu aliyekuwa mmiliki na mhariri mkuu wa gazeti la Kasi Mpya (sauti ya umma), alionekana mara ya mwisho usiku wa kifo chake akiwa na maofisa wa polisi na usalama katika baa iitwayo Cross Park katika eneo la Igoma.


“Tarehe 3 Januari, maiti ya mwandishi Issa Ngumba iliokotwa katika pori la mlima Kajuruheta, kijiji cha Mhange, wilayani Kakonko katika mkoa wa Kigoma.Ngumba alikuwa mwandishi wa habari wa Redio Kwizela. Tangu mwezi uliopita Machi, mwandishi wa habari Erick Kabendera anayeishi Dar es Salaam, anaishi kwa wasiwasi. Wazazi wake waishio Bukoba, wamehojiwa na ‘ofisa usalama’ kwa kile kilichoitwa ‘uhalali wa uraia wao.’


“Kuuwawa kwa aliyekuwa mwandishi wa habari wa Kituo cha Luninga cha ITV, John Lubungo ambaye alikuwa mfuatiliaji mahiri wa habari zinazohusu wafanyabiashara au biashara haramu ya dawa za kulevya ambayo inadaiwa kufanywa na watu wakubwa nchini, wakiwemo vigogo serikalini. 

Kuna orodha ndefu ya waandishi wa habari waliotishwa na wanaoendelea kutishwa; waliopigwa na polisi na askari magereza (Ukonga, Dar es Salaama) kwa tuhuma mbalimbali; waliotishiwa maisha kwa simu na hata kwa kufuatiliwa na watu wasiowafahamu.”

Kwa sababu ya uadilifu na kutopenda kujikweza, Mzee Tegambwage hakutaja shambulio la tindikali na mapanga dhidi yake na mwandishi mwenzake Saed Kubenea wa gazeti la Mwanahalisi, ambalo baadae lilifungiwa na Serikali hii ya CCM.


Mheshimiwa Spika,


Katika Maoni yake wakati wa mjadala wa bajeti ya Wizara ya Katiba na Sheria ya tarehe 3 Mei mwaka huu, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni ilielezea kwa kirefu jinsi ambavyo Serikali hii ya CCM imekuwa tishio kwa maisha ya waandishi wa habari na kwa uhuru wa habari katika nchi yetu. 

Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni ilirejeaRipoti ya Timu Maalum ya Uchunguzi Iliyoteuliwa na Baraza la Habari Tanzania (MCT) na Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) Kuchunguza Mazingira Yaliyopelekea Kuuawa kwa Mwandishi wa Habari Daudi Mwangosi Septemba 2, 2012 Katika Kijiji cha Nyololo, Wilaya ya Mufindi, Mkoani Iringa, iliyotolewa na Baraza la Habari Tanzania (MCT) na Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), taasisi mbili huru zinazojihusisha na masuala ya habari Tanzania.

Kwa mujibu wa Ripoti ya MCT/TEF, matokeo ya uchunguzi wao “... yanadhihirisha bila wasi wasi kwamba polisi kwa makusudi waliwavurumisha waandishi waliotoka Iringa wakati wakikusanya habari za shughuli za CHADEMA katika kijiji cha Nyololo.

 Zaidi ya hapo, Daudi Mwangosi mwenyewe aliuawa akiwa mikononi mwa polisi huku wakisimamiwa moja kwa moja na Kamanda (wa Polisi wa Mkoa wa Iringa SACP Michael) Kamuhanda.” Ripoti hiyo inaelezea jinsi Marehemu Mwangosi alivyouawa: “Alipoangalia nyuma, Daudi Mwangosi aliona kikundi cha polisi wakimpiga mwandishi mkuu wa gazeti la Nipashe wa Iringa, Godfrey Mushi.... Wakati mwandishi Godfrey Mushi akiwa bado anapigwa na polisi, marehemu Mwangosi aliwakimbilia akiwaomba waache kumdhuru zaidi Mushi kwa kuwa alikuwa mwandishi tu. 

Polisi hawakumsikiliza. Badala yake wakamburuta mwandishi huyo ambaye tayari alikuwa amepoteza fahamu na kumweka kwenye gari lao na wakamgeukia Daudi Mwangosi mwenyewe, wakampiga kwa nguvu mpaka akapoteza fahamu.”

Hata amri ya Mkuu wa Kituo cha Polisi Mafinga Mwampamba kuwataka askari polisi waache kumpiga marehemu Mwangosi haikusikilizwa na askari hao. Ili kujiokoa, marehemu Mwangosi alimkumbatia OCS Mwampamba na “baadaye kumwangukia miguuni mwake kuepuka kipigo zaidi.” 

Kwa mujibu wa Ripoti ya MCT/TEF, “picha za mgando zinaonyesha polisi mmoja akipiga bomu la machozi tumboni mwa marehemu Mwangosi kwa karibu kabisa.” Bomu hilo liliusambaratisha mwili wa marehemu Mwangosi aliyekufa papo hapo. Kwa sababu marehemu Mwangosi alikuwa chini ya miguu ya OCS Mwampamba, “naye pia alijeruhiwa vibaya.”

Mheshimiwa Spika,


Sio MCT/TEF pekee zilizofanya uchunguzi wa mauaji ya Marehemu Mwangosi. Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora nayo ilitoa Taarifa ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora ya Uchunguzi wa Tukio Lililopelekea Kifo cha Daudi Mwangosi Kilichotokea Septemba 2, 2012 Kijijini Nyololo, iliyobaini kwamba Marehemu Mwangosi “... alizingirwa na askari, aliteswa na hatimaye ... alipigwa bomu na kufa papo hapo.” Aidha, kwa mujibu wa Taarifa hiyo, “... 


Tume imejiridhisha kuwa tukio la lililopelekea kifo cha Daudi Mwangosi limegubikwa na uvunjwaji wa haki za binadamu na ukiukwaji wa misingi ya utawala bora.” Taarifa ya Tume inafafanua kuwa, “... 


Tume imejiridhisha kuwa Jeshi la Polisi limevunja haki ... ya kuishi, haki ya kutoteswa na kupigwa, haki ya usawa mbele ya sheria na haki ya kukusanyika na kutoa maoni.”

Mheshimiwa Spika,


Inaendelea..
 
Spika amesitisha bunge hilo ili kupata muda wa kuipitia hotuba hiyo kuondoa kauli za uchochezi.

AUDIO:Bofya PLAY
TUPE MAONI YAKO

TIMU YA TAIFA YA OLIMPIKI YA TANZANIA YAWASILI KWENYE KIJIJI CHA MICHEZO HIYO, STRATFORD-LONDON

 Timu ya Tanzania ya Olimpiki, imewasili kwenye kijiji cha michezo ya Olimpiki kilichopo Stratford, London, ikitokea kwenye mji wa Bradford.  Timu hiyo ya Tanzania, iliweka kambi ya mazoezi katika Chuo Kikuu cha Bradford tangu walipowasili nchini Uingereza wiki mbili zilizopita, ikiwa tayari kuiwakilisha Taifa katika michezo hiyo ya Olimpiki 2012.  Timu hiyo ilipokelewa na Balozi wa Tanzania, nchini Uingereza, Mheshimiwa Peter Kallaghe na maofisa wengine wa Ubalozi na kusindikizwa moja kwa moja kwenye kijiji cha michezo hiyo kilichopo Stratford, ikiwa tayari kwa maandalizi na ufunguzi rasmi wa michezo hiyo utakaofanyika siku ya Ijumaa 27/07/2012 hapa London.
Pichani, Balozi wa Tanzania, Mheshimiwa Peter Kallaghe akiwa pamoja na Wanamichezo hao watakaoiwakilisha Taifa mwaka huu katika Michezo hiyo ya Olimpiki nchini Uingereza.
TUPE MAONI YAKO

Bia ya Kilimanjaro yakutana na Wahariri wa Michezo kuzungumzia uzinduzi wa kampeni mpya ya 100% Tanzania Flava jijini Dar leo

 Meneja wa Bia ya Kilimanjaro,George Kavishe akizungumza na Wahariri wa Habari za Michezo (hawapo pichani) kwenye ukumbi wa mikutano wa hoteli ya New Afrika,Jijini Dar es Salaam asubuhi hii wakati wa semina ya siku moja ya inayohusu uzinduzi wa kampeni mpya ya Bia hiyo ifahamikayo kama 100% Tanzania Flava.
Meneja wa Habari wa Kampuni ya Executive Solutions ambao ndio waandaaji wa Semina ya Wahariri wa Habari za Michezo,Mike Mukunza akizungumza na Wahariri hao asubuni hii.
 Mhariri wa Habari za Michezo wa Gazeti la Champion,Saleh Ali akichangia mada katika Semina hiyo.
Mhariri wa Habari za Michezo wa Radio One,Maulid Kitenge akichangia mada katika Semina hiyo.
 Baadhi ya Wahariri wa Habari za Michezo wakiwa kwenye Semina hiyo asubuhi hii.
TUPE MAONI YAKO

Translate

 
Support : mpekuzi | John mpekuzi | Wataalam
Copyright © 2009. MPEKUZI - All Rights Reserved
Template designed by mpekuzi
Proudly powered by Blogger